Inasaidia URL Upload 🌐

Hifadhi Salama. Ingiza Kipato.

Acha kugawa maudhui yako bure. Pakia faili zako hata kwa kutumia link (URL Upload), weka bei yako, na uanze kulipwa moja kwa moja kupitia M-Pesa au Tigo Pesa papo hapo.

✓ Lipwa Papo Hapo✓ Usalama wa 100%✓ Hakuna Makato Fiche
Drive / Movie_Uploads ● Inapakia

📁 Folder 01

Tayari

🎬 Action_Movie.mp4

Inasubiri
...
Remote Upload: URL_Movie.mkvInapakia...

Uhuru wa Kuhifadhi. Nguvu ya Kuuza.

Tumetengeneza jukwaa moja linalomaliza changamoto zote za usambazaji na uuzaji wa maudhui mtandaoni.

🛡️

Usalama Unaoaminika

Faili zako zinalindwa kwa teknolojia ya juu. Wewe pekee ndiye unayeamua nani aone au apakue.

🌐

Pakia Kwa Link (URL Uploader)

Okoa bando lako! Hamisha faili moja kwa moja kutoka link yoyote mtandaoni kuingia kwenye Drive yako kwa sekunde.

💸

Pesa Yako, Muda Huo

Hatusubirishi mapato yako. Mteja akilipa kwa M-Pesa/Tigo Pesa, pesa inasoma kwenye akaunti yako hapohapo.

🚀

Kasi Isiyo na Mipaka

Pakia na pakua faili kubwa za GB nyingi kwa kasi ya ajabu bila kukwamakwama.

🔒 Picha za Harusi - Album TSh 15,000

🖼️ Picha Kuu

Picha 45

🎬 Video Full

1.2 GB
Mteja analipia hapa 👇Lipia kwa M-Pesa

Mteja Anaamini Anachokiona. Wewe Unapata Faida.

Tumeondoa wasiwasi wa wateja kwenye kununua vitu mtandaoni. Mfumo wetu unamruhusu mteja kuona majina na idadi ya faili zilizo ndani ya folder lako kabla hajalipia.

  • ✓ Anaona folder, lakini hawezi kupakua hadi alipe.
  • ✓ Malipo yanafanyika kirahisi kupitia simu (STK Push).
  • ✓ Unatoa pesa yako muda wowote kwenda kwenye namba yako.
Tengeneza Akaunti Bure →

Gharama Rafiki na za Uwazi

Chagua nafasi inayoendana na ukubwa wa biashara au mahitaji yako. Utalipia kwa siku 30 na hakuna makato ya siri.

i
Taarifa Muhimu Kuhusu Ku-RenewKifurushi chako cha siku 30 kikiisha, utahitaji kukilipia upya. Gharama ya ku-renew haipandi (inabaki ileile). Tafadhali hakikisha unalipia kwa wakati ili kulinda faili zako zisifutwe kwenye mfumo.
1 GB
TSh 100
  • ✓ Siku 30 za Uhifadhi
  • ✓ Bei ileile wakati wa Renew
  • ✓ Pakia kwa URL Inapatikana
  • ✓ Mfumo wa Kuuza Faili
Anza na 1 GB
100 GB
TSh 10,000
  • ✓ Siku 30 za Uhifadhi
  • ✓ Bei ileile wakati wa Renew
  • ✓ Pakia kwa URL Inapatikana
  • ✓ Mfumo wa Kuuza Faili
Anza na 100 GB
200 GB
TSh 20,000
  • ✓ Siku 30 za Uhifadhi
  • ✓ Bei ileile wakati wa Renew
  • ✓ Pakia kwa URL Inapatikana
  • ✓ Mfumo wa Kuuza Faili
Anza na 200 GB
500 GB
TSh 35,000
  • ✓ Siku 30 za Uhifadhi
  • ✓ Bei ileile wakati wa Renew
  • ✓ Pakia kwa URL Inapatikana
  • ✓ Mfumo wa Kuuza Faili
Anza na 500 GB

Maswali Yanayoulizwa Sana

Je, ninaweza kutoa pesa yangu muda wowote?

Ndiyo, hatusubirishi mapato yako. Unaweza kuomba kutoa fedha zako wakati wowote na zitaingia moja kwa moja kwenye namba yako ya simu uliyosajili au uliyochagua.

Kifurushi changu cha GB kikiisha faili zangu zinafutwa?

Hazifutwi papo hapo. Tunakupa muda wa nyongeza (Grace period) wa siku 3 ili ulipie tena. Utaendelea kulipia gharama ileile uliyojiunga nayo. Usipolipia ndani ya muda huu, faili zako zitafutwa.

Pakia kwa URL inafanyaje kazi?

Ni rahisi sana! Badala ya kudownload faili kwenye simu yako kisha kuli-upload kwetu (ambayo itakula bando mara mbili), wewe unaweka tu Link (URL) ya hilo faili mtandaoni. Mfumo wetu utalivuta na kuliweka kwenye Drive yako haraka sana.

Malipo yanafanyikaje kwa mteja?

Wakibonyeza "Nunua", wanaweka namba ya simu na kupokea ujumbe kwenye simu yao (STK Push) wa kuingiza PIN ya M-Pesa, Tigo Pesa au Airtel Money. Wakikamilisha, faili zinafunguka zenyewe.

Muda ni Pesa. Anza Sasa.

Ungana na maelfu ya wabunifu na wafanyabiashara wanaotumia mfumo wetu kuhifadhi na kuingiza kipato kila siku.

Anza Kutengeneza Pesa Sasa